Ohms Law Montana atingisha wavu
Kelvin Omondi ni msanii aliyezaliwa Machi 19,1992 na kulelewa katika maeneo ya Kisauni – Kaunti ya Mombasa katika familia ya vijana 4. Kulingana na juhudi zake za muziki,ameweza kuwa mshidi katika tuzo mara kadhaa hapa Pwani na hili lilichangia sana jina lake kung’aa kama mwezi kila kona ya nchi.
Nyota yake ilianza kung’aa mwaka wa 2015,baada kuachilia ngoma kali kwa jina ‘Masela wangu’ iliyorekodiwa katika studio za Stantmastaz Records chini ya producer Petrooz, na video kufanywa ni ‘Beewaxx/Stantmastaz’ chini ya ufundi wa Billy Ogada Otieno.
Mnamo Januari 14,2020 – vijana 10 katika kampeni ya ( Acha Gun Shika Mic ) iliyoanzishwa ni Ohms Law Montana waliweza kupata ufadhili kutoka mashirika tofautitofauti.
Baada ya mafanikio haya yote,niliweza kumtafuta Ohms Law Montana ili niweze kufahamu japo mambo kidogo kumhusu,kwa kuwa nyimbo zake nyingi ni kuhusu Amani…..Je,kuna jambo lolote ambalo lilimkuta ndipo akaanza kuimba na kuwahamasisha vijana kuhusu kampeni za ‘Acha Gun Shika Mic’?
Safari ya kukutana na Montana imeiva jo!
Inakuaje Montana?
Montana – Poa poa …
Mbogi inakuaje?…
Montana – Fiti sana jo!
Hivi,hizi tetesi za kuwa wewe ulikuwa street boy – na kufanya ma crime mtaani?
Montana – Yaaaa! Mhhhhh! …. Yah – its tru bana! Kuna time buda nilikuwa mbaya sana,nilikuwa mcrime sana but kuna day nili-realize kuwa sikuwa nikifanya poa kupora watu…ndo nikaamua tu kuingia kwa usanii…that’s when niliona changes…yah!
Na mbona ukaimba ‘acha gun shika mic’ kwani ulikuwa na gun b4
Montana – nuh … sikuwai kuwa na gun b4 but,hii idear after nimereform niliamua kuteach ma youths mtaani thro’ rap … juu ni vijana mob hupenda hii type of music….
Baada ya kuchapa gumzo fupi na Montana,aliniachia playlist ya baadhi ya track zake …
Masela Wangu – OHMS LAW MONTANA
Poleni feat. Simple Boy – OHMS LAW MONTANA
Wamakata Imara – OHMS LAW MONTANA
Winfrey Vennesa – OHMS LAW MONTANA
Make a name – Odinareh bingwa feat. Ohm’s Law Montana
Gava yangu – OHMS LAW MONTANA
YOUNG WILD & NASTY – OHMS LAW MONTANA
Sirens – Kassamoney feat. Dizasta & Ohm’s law Montana
ABIRO KUOMIOHMS – LAW MONTANA
Vile vile Montana amekiri kuachilia Album mpya hivi karibuni,kuhusu covid-19 na issue zingine…
Stay safe!
Stay tuned!