SERIKALI YA KITAIFA IWEKE MIKAKATI YA KUZIPA CHAKULA FAMILIA MASIKINI ASEMA MWAKILISHI WA WADI YA MKONGANI
Serikali ya kitaifa imetakiwa kuweka mikakati mwafaka itakayohakikisha wananchi wanaotoka katika familia maskini wanapata chakula wakati huu ambapo serikali imetoa marufuku ya kutotoka nje.
Mwakilishi wa wadi ya Mkongani kaunti ya Kwale Ndoro Mweruphe amesema iwapo serikali inataka kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Corona basi infaa kutekeleza mpango huo.
Mweruphe amesema tayari baadhi ya mataifa ambayo yaliweka marufuku ya kutotoka nje wamesambaza chakula kwa wananchi wao na hali hiyo imepunguza virusi hivyo katika mataifa hayo.
Wakati uo huo ameongeza kuwa bunge la kaunti ya Kwale limesitisha shughuli zake hadi hali itakaporejea kuwa shwari.