
WAKAAZI WA MOMBASA WAHIMIZWA KUSHIRIKI VIKAO VYA UMMA
Spika wa bunge la kaunti ya Mombasa Harub Khatri amewataka wakaazi wa kaunti hiyo kushiriki kikamilifu vikao vya umma vinavyolenga kujadili maswala ya bajeti na ushuru katika kaunti ya Mombasa.
Akizungumza mjini Mombasa, Harub amesema mara nyingi wakaazi wa Kaunti hiyo hupuuza vikao hivyo na baadaye kulalamikia kutozwa kodi ya juu na Serikali ya Kaunti hiyo.
Harub ameshikilia kwamba ni sharti kuwepo na majadiliano kati ya wakaazi na serikali ya kaunti hiyo akisisitiza umuhimu wa wakaazi kuhudhuria vikao vya kujadili kuhusu maswala ya ushuru, maendeleo na uchumi wa Kaunti hiyo.
Kauli yake imejiri baada ya mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir kulalamikia ushuru wa juu unaotozwa wakaazi wa kaunti ya Mombasa.