Pamba ya BT ina mazuri gani?
Baraza la mawaziri nchini limepitisha kutumika kwa pamba aina ya BT humu nchini katika juhudi za kuimarisha zao la mmea huo. Hatua hii inajiri baada ya pamba aina ya bt kufanyiwa majiribio shambani kwa muda wa miaka mitano.
Katika kikao hicho kilichoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta, kupitishwa kwa utumizi wa bt kumetajwa kama hatua kuu mojawapo itakayoimarisha nguzo za ajenda kuu nne humu nchini ambazo Rais amekuwa akizipa kipaumbele.
Pamba aina ya bt ipo na uwezo wa stahamili wadudu waharibifu na huzaa kiwango kikubwa cha pamba. Hali hii itaimarisha viwanda vya utengenezaji nguo humu nchini.