Vifaa vya kuhesabu watu vyaibiwa Likoni, mtu mmoja apigwa faini kwa kukataa kuhesabiwa
Vifaa vitatu vinavyotumika kukusanya takwimu katika zoezi linaloendelea la kuhesabu watu vimeibwa katika eneo la Likoni Kaunti ya Mombasa.
Kamishna wa Kaunti hiyo Gilbert Kitiyo amesema mmoja wa Maafisa hao alivamiwa na genge la watu nyakati za usiku na kunyang’anywa kifaa kimoja, huku vingine viwili vikiibwa katika nyumba ya makaazi ya Maafisa wengine wawili akisema tukio hilo linachunguzwa.
Hata hivyo licha ya baadhi ya changamoto hizo, zoezi hilo linaendelea vyema katika Kaunti hiyo na kufikia sasa asilimia 80 ya Wakaazi wa Kaunti hiyo wamehesabiwa.
Akizungumza Mjini Mombasa mapema leo, Kitiyo amehimiza ushirikiano ili kulifanikisha zoezi hilo, akiwataka Wakaazi watakaoachwa nje ya zoezi hilo kuripoti kwa Maafisa tawala ili wahesabiwe.
Zoezi hilo la sensa linakamilika siku ya Jumamosi juma hili.