KWASCO yashindwa kusukuma maji kutokana na kukatiwa umeme
Taarifa na Amina Fakii
Usimamizi wa kampuni ya usambazaji maji kaunti ya Kwale (KWASCO), imeweka wazi kuwa imekatiwa umeme kufuatia malimbikizi ya madeni inayodaiwa na kampuni ya Kenya Power.
Mwenyekiti wa bodi inayosimamia kampuni hiyo ya maji Francis Nzai amesema tangu mwezi wa Januari mwaka huu, kampuni hiyo inawadai wateja wake takraban shilingi milioni 14, hali ambayo imepelekea kushindwa kulipa madeni yake.
Hata hivyo Nzai amesema ili kuafikia malengo ya kampuni hiyo ya kutoa huduma bora za maji, ni lazima ikusanye fedha zaidi ya shilingi milioni 13 kila mwezi lakini kwa sasa kampuni hiyo inakusanya shilingi milioni 7 hadi 8 kutoka kwa wateja wake.
Wabunge waikosoa bajeti
Taarifa na Rasi Mangale
Wabunge wa bunge la kitaifa walioshuhudia kosomwa kwa bajeti bungeni wameikosoa.
Wakiozwa na Mbunge wa Shinyalu Justus Kizito wa bunge hao wameikosoa bajeti hio wakisema haijaangazia ipasavyo wakulima wa humu nchini.
Kizito aidha amepongeza hatua ya kuongezewa ushuru wa michezo ya Kamari kwa asilimia 10.
Kwa upande wao wahudumu wa bodaboda mjini kwale wametoa hisia mseto kuhusu suala la leseni za udereva lilioangaziwa katika bajeti hio ambapo muda wa leseni umeongezwa kutoka miaka 3 hadi mitano na ada za leseni hizo kuongezwa.
“Deni la taifa limethibitiwa,” asema waziri wa fedha
Waziri wa fedha nchini Henry Rotich amesoma bajeti ya kitaifa ya shilingi trilioni 3 kwa ajili ya matumizi ya mwaka wa kifedha 2019/2020.
Akisoma bajeti hiyo waziri Rotich amesema kuwa deni la taifa ambalo kwa sasa limefikia shilingi trilioni 5.3 linadhibitiwa,huku akizitaka serikali za kaunti kutoidhinisha miradi mipya badala yake kukamilisha miradi ilioanzishwa hapo awali.
Katika bajeti hiyo Rotich amesema shilingi bilioni 326 zimetengewa idara ya usalama huku bilioni 2.9 zikitengewa taasisi za kupambana na ufisadi nchini ikiwemo tume ya EACC na afisi ya mkurugenzi wa mashataka ya umma ili kufanikisha vita dhidi ya ufisaidi.
Shilingi bilioni 450.9 zimetengewa mpango wa agenda nne kuu za serikali,shilling bilioni 314 zikielekezwa kwa serikali za kaunti kote nchini huku idara ya nyumba ikitengewa shilingi billion 10.5.
Katika sekta ya elimu shilingi bilioni nne zimetengwa kugharamia ada za mitiani ya kitaifa ya KCPE na KSCE kwa wanafunzi wa humu nchini huku shilling billion 3.2 zikitengwa kuajiri waalimu zaidi, sekta ya afya ikitengewa kima cha shilling billion 47.8.
Vile vile awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR umetengewa billioni 55.5, hazina za vijana,wanawake na watu wanaoishi na ulemavu ikitengewa bilioni moja huku sekta ya michezo na sanaa ikitengewa shilingi bilioni 7.9.
Kituo cha polisi chafunguliwa Mjambere
Idara ya usalama imefungua rasmi kituo cha polisi eneo la Mjambere huko Kisauni kaunti ya Mombasa.
Akizungumza na wanahabari baada ya kufungua kituo hicho mapema hii leo kamishana kaunti ya Mombasa Evans Achoki amesema kituo hicho kitasaidia pakubwa kuimarisha usalama katika eneo bunge la kisauni.
Achoki amesema mikakati imeekezwa kukabili magenge ya wahalifu yanayoangaisha wakaazi wa kisauni na kaunti ya Mombasa kwa jumla.
Kaunti ya Kilifi kukumbwa na ongezeko la kupe, madakatari wa mifugo waonywa
Idara ya mifugo kule Malindi kaunti ya Kilifi imewataka wakulima wa mifugo kuhakikisha kuwa wanawapeleke mifugo wao kwenye Josho ili kuepukana na magonjwa msimu huu wa mvua.
Kwa mujibu wa daktari mkuu wa mifugo eneo la Malindi Godric Mwaringa huenda kukashughudiwa ongezeko la kupe hali ambayo huenda ikahatarisha hata zaidi mifungo.
Mwaringa anadai kuwa jumla ya majosho manne yamesambaratika kwa sasa kule Malindi pekee hivyo kutatiza wakulima.
Ameongeza kuwa mengi ya majosho yanakumbwa na changamoto ya maji sambamba na namna ya kufikiwa na wakulima hivi sasa kutokana na wakulima wa mahindi kuziba njia ambazo hutumiwa kupitsha mifugo hadi kwa josho hizo.
Miongoni mwa maeneo ambako majosho hayatumiki ni pampja na Jilore, Kijiwetanga, Kakuyuni sambamba na Viriko.
MUHURI yataka majaji kuchunguzwa
Taarifa na Sammy Kamande
Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la MUHURI linataka majaji watatu wa mahakama ya Rufaa Erastus Githinji, Martha Koome na Fatuma Sichale kuchunguzwa kufuatia uamuzi wao wa kupinga kesi iliyowasishwa na shirika hilo kuhusu uteuzi wa makarani 290 waliyosimia marudio ya uchaguzi wa urais mwaka wa 2017.
Mwenyekiti wa shirika hilo Khelef Khalifa amesema kwamba majaji hao watatu hawakuzingatia sheria yoyote na walifanya hivyo baada ya kuongozwa na aliyekuwa rais wa mahakama hiyo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa sheria nchini Paul Kihara.
Kulingana na Khalifa, misingi ya katiba ilipuuzwa kwani Majaji hao hawakuwa pamoja wala hawakuianisha uamuzi wowote ule bali walikabidhiwa uamuzi huo wa kupinga uamuzi wa Jaji wa mahakama kuu George Odunga aliyeweka wazi kwamba uteuzi wa Maafisa hao na Manaibu hao ulifanywa kinyume cha sheria.
Khalifa ametaka tume ya huduma ya mahakama nchini JSC kuwachunguza Majaji hao watatu anaodai wanatumiwa na Wanasiasa katika kutekeleza majukumu yao badala ya kuzingatia sheria na kuwatendea Wananchi haki.
Kwa sasa Shirika hilo limeapa kuwasilisha kesi hiyo mahakamani ili kushinikiza kuchukuliwa hatua kwa Majaji wa mahakama ya rufaa Erastus Githinji, Martha Koome na Fatuma Sichale kufuatia uamuzi wao tata wa kuruhusu Maafisa 290 waliyoteuliwa na tume ya IEBC kusimamia marudio ya uchaguzi wa urais mwaka 2017.
Wanawake wawili wanaswa na misokoto ya bangi 2600 Kilifi
Taarifa na: Ephie Harusi
Kilifi, Kenya, Juni 11 – Wanawake wawili wanazuiliwa katika kituo cha polisi mjini Kilifi baada ya kupatikana na zaidi ya misokoto elfu 2600 ya bangi katika operesheni inayoendelezwa dhidi ya walanguzi wa mihadarati katika kaunti hiyo.
Akithibitisha kukamatwa kwao afisa mkuu wa polisi Kilifi kaskazini Patrick Njoroge amesema polisi wamepashwa habari na wananchi na kufanikiwa kuwanasa washukiwa na bangi hiyo yenye thamani ya shilingi 300,000.
Njoroge amesema polisi wataendelea na oparesheni ya kuwasaka walanguzi wa mihadarati kuhakikisha biashara hio inasambaratishwa kaunti nzima ya Kilifi.
Wavuvi waonywa dhidi ya kutumia vifaa visivyo halali kuvulia samaki
Taarifa na Charo Banda.
Malindi Kenya, Juni 8 – Wavuzi katika eneo la Cha fisi huko Watamu kaunti ya kilifi sasa wametakiwa kufuatia sheria za uvuvi ili kukomesha mizozo ya mara kwa mara baina yao na maafisa wa shirika la KWS katika eneo hilo.
Hii ni baada ya kubainika kuwa asilimia kubwa ya wavuvi katika fuo za bahari ya hindi wanashiriki uvuvi haramu na ambao haukubaliki na KWS.
Akiongea na takriban wavuvi 300 mbunge wa Kilifi kazkazini Owen Baya amesema kuwa wavuvi wengi katika eneo hilo wamekuwa wakinaswa na maafisa wa KWS kwa kutumia vifaa bandia kuvua samaki.
Kulingana na afisaa mkuu wa KWS tawi la Watamu Daddly Tsinyau wavuvi wengi eneo hilo hawazingatii uvuvi unaofaa na kwamba hutumua nyavu bandia ambazo zinaathiri vibaya mazingira.
Mashirika ya kijamii kuungana kupinga nyongeza ya mishahara ya Wabunge
Taarifa na Alphalet Mwadime.
Watetezi wa haki za kibinadamu Ukanda wa Pwani wataungana na wenzao kutoka sehemu nyingine za nchi kuandama ili kuwashinikiza Wabunge kuwachana na azma yao ya kupigania nyongeza ya mishahara.
Afisa wa maswala ya dharura katika Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu nchini la Haki Afrika Mathias Shipetta amesema kwamba bila ya watetezi hao kushirikiana na wananchi na kufanya harakati hizo iwapo mwananchi mashinani atazidi kukandamizwa na wabunge hao walafi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Hussein Khalid amekariri kwamba tayari Shirika hilo linashirikiana na watetezi wengine wa haki za kibindamu ili kulijadili swala hilo na Wabunge wa eneo la Pwani ili kuwashinikiza kulitupilia swala hilo.