Picha kwa hisani –
Wizara ya Afya nchini imewahimiza wakenya kuendelea kuzingatia kikamilifu masharti ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona ili kudhibiti usambazaji wa virusi hivyo.
Katibu mkuu msimamizi katika Wizara hiyo Dkt Rashid Aman amesema ni muhimu kwa kila mkenya kuchukua jukumu hilo hasa kwa kuzingatia usafi wa mazinmgira, kuosha mikono kila mara, kuvaa barakoa na kutumia vieuzi.
Akigusia takwimu za maambukizi ya virusi vya Corona, Dkt Aman amesema idadi ya maambukizi nchini imefikia watu 34,705 baada ya watu 212 kuthibitishwa kupata maambukizi hayo kutokana na sampuli 3,937.
Dkt Aman amesema kati ya watu hao 212, wakenya ni 198 huku watu 14 wakiwa raia wa kigeni na wanaume ni 132 huku wanawake wakiwa 80 na mtoto wa mwezi mmoja ni miongoni mwa walioambukizwa.
Hata hivyo amedokeza kuwa watu 195 wamethibitishwa kupona virusi hivyo na idadi hiyo kufikia watu 20,644 huku watu wanne wakiaga dunia.