Story by our correspondent
Baadhi ya wazee wa jamii ya wamijikenda kanda ya Pwani wamejitokeza na kushinikiza ushirikiano wa jamii hiyo ili kuhakikisha wanapigania raslimali za Pwani ikiwemo misitu ya Kaya, ardhi na ajira.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha wazee wa Kaya za mijikenda Mwinyi Mwalimu Mbisho, wazee hao wamesema kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia ushawishi wao kuikandamiza jamii ya wamijikenda.
Naye Grace Mbodze anayewakilisha jinsia ya kike katika chama hicho ameitaka serikali kuingilia kati na kuhakikisha jamii ya wamijikenda inatambulika katika ngazi zote za serikali ili kunufaika miradi ya maendeleo inayoidhinishwa na serikali.
Kwa upande wake Kiongozi wa vijana wa jamii ya wamijikenda Nguma Charo amewataka mawaziri Salim Mvurya, Aisha Jumwa na Spika Amason Kingi, kuhakikisha wanawabijikia majukumu yao kutatua changamoto zinazowakumba ikiwemo swala tata la Ardhi.