Story by: Ali Chete.
Mahakama ya Mombasa imewahukumu kifungo cha nje cha miezi sita wanaharakati 5 wa mashirika ya kuteteta haki za binadamu pamoja na kondakta mmoja wa matatu.
Sita hao ni pamoja na Francis Auma wa shirika la MUHURI, Lucas Fondo, Tirus Mukami, Nato Michael, Felix Otieno na Kiti Nyale ambaye ni utingo walikamatwa na kushtakiwa mwaka wa 2020 kwa kosa la kuvunja sharia za kudhibiti msambao wa virusi vya Corona walipokuwa wakiandamana kulalamikia ufujaji wa pesa za umma zilizotengwa kukabiliana janga hilo.
Picha Kwa Hisani.
Akitoa uamuzi huo, hakimu Ritah Amwayi amesema kuwa sita hao walifeli kuzingatia sheria ziliwekwa na serikali kudhibiti msambao wa virusi hivyo.
Wakizungumzia hukumu hio wanaharakati kaunti ya Mombasa wakiongozwa na mwenyekiti wa shirika la MUHURI Khelef Khalifa wamesema watakata rufaa kupinga uamuzi huo.
Picha Kwa Hisani.
Kwa upande wake naibu mkurugenzi wa shirika la Haki Africa Bi Salma Hemed amesema hatua hiyo khaiwezi kuwazuia wanaharakati kuandamana kulalamikia utepetevu wa serikali.