Picha kwa hisani –
Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna amesema mchakato unaoendelezwa na baadhi ya wanasiasa wa pwani wa kuunda chama kipya cha kisiasa cha pwani hautafaulu.
Akizungumza na wanahabari Sifuna amesema sheria za nchi haziruhusu kubuniwa kwa vyama vya kisiasa vya eneo moja,akisema chama cha ODM ndio chama pekee kinachopigania maslahi ya wakaazi wapwani.
Sifuna aidha amesema ni lazima viongozi walio wanachama wa chama cha ODM wazingatie sheria za chama hicho na kwamba wale watakaoenda kinyume na sheria hizo watachukuliwa hatua za kinidhamu.