Picha kwa hisani –
Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu nchini MUHURI linaitaka Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kukabidhi shirika hilo habari zote muhimu zinazofungamana na mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba na BBI.
Mwenyekiti wa shirika hilo Khelef Khalifa amempa Mwenyekiti wa Tume hiyo siku saba kutoa orodha ya majina ya watu wote waliyotia saini zilizowezesha kuidhinisha ripoti ya BBI.
MUHURI vile vile imetaka IEBC kutoa gharama ya zoezi la ukusanyaji saini na ya kura ya maamuzi inayopangwa na kuweka bayana fedha za zoezi hilo zitakakotolewa na iwapo fedha hizo zilipitishwa na bunge la kitaifa na Wizara ya fedha.
Katika barua hiyo ambayo tayari imekabidhiwa Mwenyekiti wa IEBC MUHURI inataka kufahamu tarehe ya mwisho tume hiyo iliwasajili wapiga baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa mwaka wa 2017.