Picha kwa hisani –
Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko hii leo anatarajiwa kujua hatma yake iwapo ataendelea kuhudumu kama gavana ama atatimuliwa.
Sonko anatarajiwa kufika mbele ya bunge la seneti kujitetea dhidi ya tuhma zinazomkabili ikiwemo matumizi mabaya ya mamlaka na ubadhirifu wa fedha za umma.
Hii ni baada ya bunge la kaunti kupiga kura za kutokuwa na imani na Sonko wiki jana na kumtimua kwa kile walichotaja kama ubadhilifu wa fedha za umma na utumizi mbaya wa mamlaka.