Picha kwa hisani –
Chifu wa lokesheni ya Golini katika eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale Ali Matsudzo amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kulingana na naibu chifu wa eneo hilo Changoma Mbwana, marehemu alifariki jana jioni katika hospitali ya Kwale baada ya hali yake ya afya kudorora.
Mbwana amesema kuwa chifu huyo alikuwa akiugua magonjwa tofauti yakiwemo kisukari na shinikizo la damu kwa muda sasa.
Hata hivyo, Kamishena wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo amekanusha madai ya kuwa chifu huyo amefariki kutokana na ugonjwa wa corona.
Ngumo amesema licha ya chifu huyo kugonjeka, chanzo cha kifo chake hakijabaika baada ya ripoti kamili kutolewa na madaktari.
Marehemu atazikwa leo nyumbani kwao mwendo wa saa saba mchana katika eneo la Ziwani.