Picha kwa hisani –
Muuguzi mmoja amefariki katika hospitali kuu ya Ukanda wa Pwani baada ya kuambukizwa virusi vya Corona.
Bi Margaret Mwadime amekuwa akihudumu katika hospitali hiyo kwa muda mrefu na aliambukizwa Virusi hivyo akiwa kazini .
Kulingana na Gavana wa Kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho, Bi Mwadime amekuwa akipokea matibabu ya dharura katika kituo cha kuwatibu wagonjwa wa Corona katika hospitali kuu ya Ukanda wa Pwani.
Muuguzi huyo ni wa pili kufariki katika hospitali hiyo kuu ya Ukanda wa Pwani, huku wengine sita wakiwa hali mahututi hospitalini humo baada ya kuambukizwa virusi vya Corona.