Picha kwa Hisani –
Kutokana na ongezeko la visa vya dhulma za kijinsia katika kaunti ya Kwale, sasa buneg la kaunti hiyo limeipa Wizara ya Afya ya kaunti hiyo jukumu la kuidhinisha kitengo maalum cha kushughulikia visa hivyo.
Mwakilishi wa wadi ya Mwereni katika kaunti ya Kwale Manza Beja, amesema Wizara hiyo inafaa kuhakikisha inaidhinisha kitengo hicho katika hospitali zote kuu za kaunti hiyo ili kuwapa nguvu waathiriwa kuwasilisha lalama zao.
Manza amesema kitengo hicho kitahakikisha visa hivyo vinapungua kwa asilimia kubwa huku akisema kama viongozi watashirikiana na wadau mbalimbali kudhibiti visa hivyo katika kaunti ya Kwale.
Wakati uo huo amependekeza serikali kuu kuidhinisha kitengo cha kushuhulikia visa vya dhulma za kijinsia katika kila kituo cha Polisi katika kaunti hiyo sawia na kuteua afisa maalum wa polisi kuchukua jukumu la kuripoti kesi hizo Mahakama na wala sio kila afisa wa polisi.