Kwenye Picha – katikati
Picha kwa Hisani –
Wakaazi wa eneo la Msambweni kaunti ya Kwale wanashikiza Tume huru ya uchaguzi nchini IEBC, kutangaza tarehe ya uchaguzi mdogo wa eneo bunge hilo.
Wakiongozwa na Mwanasiasa Hassan Chitembe, wakaazi hao wamesema kucheleweshwa kwa uchaguzi huo mdogo kumewanyima maendeleo na maswala msingi wakaazi wa eneo bunge hilo.
Chitimbe amemtaka Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga kuhakikisha anaishinikiza Tume ya IEBC kuandaa tarehe rasmi ya uchaguzi huo mdogo ili wakaazi wa eneo bunge hilo wanufaike kimaendeleo.
Kauli yake imeungwa mkono na Abdalla Mambo, aliyesema wakaazi wa eneo bunge hilo wanatatizika pakubwa kutokana na kukosekana Kiongozi wkatika eneo bunge hilo.
Shinikizo zao zimejiri baada ya kifo cha mwendazake Suleiman Dori mwezi Machi mwaka huu aliyekuwa mbunge wa eneo hilo la Msambweni.