Picha kwa Hisani –
Waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe na Katibu mkuu katika wizara hiyo Susan Mochache wamekana madai kuwa wamehusika katika uwizi wa fedha zilizotengwa kudhibiti virusi vya Corona.
Ni wiki moja sasa ambapo kumekuwa na madai kwamba maafisa katika wizara hiyo ya afya na wale wa Taasisi ya kusambaza dawa nchini Kemsa wamekuwa wakielekezeana lawama kuhusu nani wa kulaumiwa kwa kupotea kwa mabilioni ya fedha .
Katibu Mochache amekana madai kuwa aliamrisha taasisi ya Kemsa kununua baadhi ya vifaa na pia akana lawama kuwa alitoa orodha ya kampuni zinazostahili kupewa zabuni .
Kauli ya wawili hao imejiri huku wabunge katika bunge la kitaifa wakitaka serikali kusimamisha ulipaji wa fedha takrbani shilingi milioni 148 kwa kampuni ambazo zilipewa jukumu la kuagiza vifaa vya kudhibiti virusi vya Corona.
Mbunge wa Mbeere Kaskazini na pia mwanachama wa kamati ya afya bungeni Muriuki Njagagua amesema kuwa vifaa hivyo viliagizwa kwa njia zisizo halali.