Picha kwa hisani –
Idara ya mahakama nchini imezindua mfumo mbadala wa kusikiliza kesi unaohusisha njia za kitamaduni na utakaotumika kuamua kesi mbali mbali nchini pasi na wahusika kufika mahakamani.
Naibu jaji mkuu nchini Philomena Mwilu amesema kuna haja ya mabadiliko kufanywa katika utoaji huduma na haki katika mahakama za humu nchini ili kuhakikisha haki za kikatiba za wananchi zinazingatiwa.
Kwa upande wake msajili mkuu wa idara ya mahakama nchini Bi Anne Amadi amesema mfumo huo utaleta mabadiliko katika idara ya mahakama kwani utarahisisha upatikanaji wa haki na kupunguza mrundiko wa kesi mahakamani.
Kwa upande wake naibu mwenyekiti wa jopo linalosimamia utekelezaji wa mfumo huo Daktari Steve Akoth amesema kesi zinazosuluhishwa kupitia mfumo huo zitasuluhishwa kwa kuzingatia katiba.