Picha Kwa Hisani –
Watu watatu wamethibitishwa kufariki papo hapo huku zaidi ya 20 wakijeruhiwa vibaya baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani katika eneo la Tororo karibu na mtaa wa Shaurimoyo kule Vipingo kaunti ya Kilifi kwenye barabara kuu ya Mombasa -Malindi.
Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, wamesema ajali hizo zimetokea mara mbili gari mbili ndogo aina ya prado zilizokuwa zimetokea eneo la Mombasa kuelekea Kilifi zimegongana ana kwa ana na matatu mbili za abiria aina ya Nissan na nyenngine ikagongana na Lori aina ya Canter na kusababisha ajali hiyo.
Wakaazi mtaa huo wamesema waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali kuu ya kaunti ya Kilifi mjini Kilifi kwa matibabu ya dharura huku walioga dunia wakipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Kilifi.
Maafisa wa polisi waliofika katika eneo la ajali hiyo wamewataka maderava wa gari za binafsi na zile za uchukuzi wa umma kuzingatia kikamilifu sheria za barabarani ili kuepuka ajhali huku wakisema tayari uchunguzi umeanzishwa ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.