Picha Kwa Hisani –
Naibu Gavana wa kaunti ya Lamu Abdulhakim Aboud amesema visa vya wavuvi kuaga dunia wanapokua katika bahari hindi vimekithiri katika kaunti hiyo kutokana na ukosefu wa vifaa vya mawasiliano miongoni mwa wavuvi.
Akizungumza na Wanahabari kule Amu, Aboud amesema wavuvi hasa wale wanaoendeleza uvuvi katika maji makuu wanafaa kupewa vifaa hivyo ili waweze kuwasiliana na mamlaka husika wanapokumbwa na mikasa baharini.
Hata hivyo amesema serikali ya kaunti ya Lamu inaendelea na mipangilio ya kuhakikisha idara ya uvuvi katika kaunti hiyo inawapa wavuvi vifaa hivyo.
Kauli yake imejiri huku wavuvi katika kaunti hiyo wakiwa wanalalamikia kutoimarika kwa sekta hiyo kutokana na ukosefu wa vifaa vya kisasa vya kuendeleza uvuvi katika bahari hindi.