Picha kwa hisani –
Viongozi wa kaunti za Pwani wamesema ugatuzi umesaidia pakubwa mashinani katika kuboresha maswala ya maendeleo kutokana na mgao wa fedha unaotolewa na serikali ya kitaifa kwa serikali kaunti.
Wakiongozwa na Gavana wa Kwale Salim Mvurya, amesema raslimali nyingi zinazowafaidi wananchi mashinani zimetokana na uwepo wa ugatuzi huku akisisitiza umuhimu wa viongozi kutambua swala la ugavi wa mapato mashinani.
Gavana Mvurya amesema mfumo wa ugavi wa mapato unaopendekezwa na Tume ya ugavi wa mapato nchini CRA unahujumu maendeleo ya wananchi, huku akisema iwapo bunge la Seneti litapitisha mfumo huo basi serikali za kaunti hapa Pwani zitapoteza zaidi ya shilingi bilioni 5.
Kwa upande wake Mbunge wa Kilifi Kaskazimi Owen Baya ameunga mkono kauli ya Gavana Mvurya, akisema kupunguziwa fedha serikali za kaunti kutakandamiza miradi ya maendeleo mashinani.