Picha kwa Hisani
Wizara ya Ardhi katika Serikali ya kaunti ya TaitaTaveta imesema masorovea katika kaunti hiyo ndio kikwazo kikuu katika kutatua mizozo ya ardhi kwani wengi wao wanashirikiana na mabwenyenye kunyakua ardhi za umma.
Akizungumza kule Voi, Waziri wa Ardhi kaunti ya Taita taveta Mwandawiro Mghanga amesema serikali ya kaunti hiyo haitaruhusu wananchi wa eneo hilo kufurushwa katika ardhi zao.
Mwandawiro, amesema serikali ya kaunti hiyo itaendelea kupigania haki za wananchi wanaonyanyaswa ardhi zao na baadhi ya watu wachache kutokana na tamaa zao za ardhi.
Kwa muda sasa maafisa kutoka afisi ya ardhi katika kaunti hiyo wamekuwa wakilaumiwa kwa madai ya kushirikiana na mabwenyenye kughushi hati miliki za ardhi ili kuwafurusha wakaazi katika ardhi zao.