Picha kwa Hisani
Rais mstaafu wa awamu ya tatu nchini Tanzania Benjamin William Mkapa ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 81.
Rais John Pombe Magufuli ametangaza usiku wa kuamkia leo kupitia runinga ya taifa taarifa za kufariki dunia kwa kiongozi huyo wa awamu ya tatu katika hospitali moja jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Taarifa hiyo hata hivyo haikuweka wazi Mzee Mkapa alikuwa akisumbuliwa na maradhi gani ambapo magufuli amesema Mkapa atamkumbukwa kwa mapenzi yake makubwa kwa Taifa la tanzania, ucha Mungu, uchapakazi katika kujenga uchumi.
Mzee Mkapa alizaliwa Novemba 1938, Mkoani Mtwara kusini mwa Tanzania, na aliliongoza taifa hilo kwa mihula miwili toka mwaka 1995 mpaka 2005.