Mchanganuzi wa maswala ya kisiasa nchini Profesa Hassan Mwakimako, amesema mchakato wa kisiasa unaoendelea kuhushudiwa katika vyama mbalimbali nchini huenda ukachangia siasa za mapema za mwaka wa 2022.
Mwakimako amesema jinsi inavyoonekana sasa humu nchini ni wazi kuwa msimu wa kisiasa imewadia na mvutano wa kisiasa unaoshuhudiwa ni kati ya mikakati ambayo inalenga kushuhudiwa kwa mabadiliko ya kisiasa katika bunge la seneti na lile la kitaifa.
Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu, Mwakimako amesema mchakato huo wa kisiasa ni njia moja wapo ya viongozi wa kisiasa kuonyesha makali yao ndani ya vyama vyao vya kisiasa.
Wakati uo huo ameweka wazi kuwa kutimuliwa kwa baadhi ya wabunge katika kamati mbalimbali za bungeni sio ati wabunge hayo wametimuliwa katika viti vyao vya maeneo bunge.