Picha kwa hisani –
Wizara ya Afya nchini imewahakikishia wahudumu wa afya na madaktari katika kaunti ya Nairobi kuwa watapewa mazingira safi ya kazi sawia na hudumu za bima ya afya NHF.
Katibu mkuu msimamizi katika Wizara hiyo Dkt Mercy Mwangangi ameyasema hayo baada ya Muungano wa Madaktari nchini KMPDU kutoa makataa ya siku 7 kwa swala hilo kushuhulikiwa la sivyo washiriki mgomo.
Akigusia takwimu za Covid-19, Dkt Mwangangi amesema watu 580 wamethibitishwa kupata maambukizi ya virusi vya Corona kutokana na sampuli 5,458 baada ya kufanyiwa uchunguzi na idadi hiyo kuongezeka hadi watu 29,334.
Dkt Mwangangi amesema watu 530 ni wakenya huku 50 wakiwa ni raia wa kigeni na 336 wakiwa ni wanaume na 244 ni wanawake huku mtoto wa mwaka mmoja akiwa kati ya waliopata maambukizi hayo.
Hata hivyo amesema kuwa watu 198 wamethibitishwa kupona virusi hivyo na kupelekea idadi hiyo kufikia watu 15,298 huku watu 5 wakiaga dunia.