Picha kwa hisani –
Mbunge mteule wa Msambweni Feisal Abdallah Bader ameapishwa rasmi kuwa mbunge wa Msambweni katika majengo ya bunge la kitaifa kule Nairobi.
Feisal ameapishwa ramsi na Spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi baada ya kuwasilishwa mbele ya bunge hilo na Mbunge wa Lungalunga Khatib Mwashetani na viongozi wengine waliomuunga mkono katika kampeni zake.
Feisal ameahidi kuilinda Katiba ya nchi, kuwa muamini kwa nchi ya Jamhuri ya Kenya sawia na kuahidi kutekeleza majukumu yake kama mbunge kwa uamini na uadilifu.
Feisal alitangazwa rasmi kuwa mbunge mteule wa Msambweni na Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC, baada kushika uchaguzi mdogo wa Msambweni Disemba 15 mwaka huu kuwa kupata kura 15,251.